Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) leo Jumapili Oktoba 21 amefanya ziara ya kikazi katika Jiji la Dodoma ambapo alipata nafasi ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Jiji na watumishi kutoka taasisi mbalimbali zilizopo Jijini Dodoma, ambapo aliwapongeza kwa kuvuka lengo la ukusanyaji mapato ya ndani na kuwataka watumishi hao kusimamia vizuri matumizi ya fedha za serikali, kabla ya kutembelea miradi mikubwa ya ujenzi wa miuondombinu ikiwemo Stendi Kuu ya Mabasi, Soko Kuu la kisasa, na eneo la uwekezaji la Njedengwa.
Aidha, alisema amepata faida kwa kupata nafasi ya kuonana na watumishi wa umma kwa karibu na kuwakumbusha kutekeleza wajibu wao wa utendaji kazi, huku akiwakumbusha na kuwasisitiza kubadilika na kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa na kila mmoja ajue msimamo wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuwahudumia wananchi wake kwa kuimarisha utoaji huduma mbalimbali kamba vile huduma za afya, maji, elimu, kilimo, ufugaji, makazi, kutenga na kupima ardhi, na kadharika.
Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri Mkuu alipata nafasi ya kutembelea na kufungua ofisi kuu ya kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Makutupora na baadaye kutembelea kiwanda cha kusindika zabibu cha Alko Vintage kilichopo eneo la Makole ambapo alikagua uzalishaji wa mvinyo.
Baada ya hapo msafara wa Mhe. Waziri Mkuu ulitembelea maeneo ya Nzuguni na kuona shughuli za ujenzi wa Standi kuu ya mabasi na Soko kuu la nafaka na mbogamboga na kisha kwenda kuzindua mradi wa maji eneo la uwekezaji mkubwa lililopo Njedengwa.
Mhe. Waziri Mkuu alikuwa akihitimisha ziara yake ya kuutembelea mkoa wa Dodoma kwa kutembelea wilaya ya Dodoma, ambapo awali alitembelea Wilaya za Kondoa, Chemba, Mpwapwa, Kongwa, Bahi na Chamwino ambapo alikagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) alipotembelea Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Makutupora na kufungua ofisi kuu ya Kikosi. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Godwin Kunambi
Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo ya ramani na mchoro wakati wa ziara yake leo Oktaba 21, 2018 kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipango miji Joseph Mafuru.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.