Zoezi la kujiandikisha na kuboresha taarifa za wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura limekamilika leo katika Jimbo la Dodoma mjini baada ya zoezi hilo kuongezewa muda wa siku moja kutokana na idadi kubwa ya wananchi waliokuwa wakijitokeza jijini hapa.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Wilson Mahera amepongeza jinsi zoezi hilo lilivyoendeshwa jijini Dodoma na kuwashukuru wananchi pamoja na watendaji wote walioshiriki kufanikisha zoezi hilo. Katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa Mkurugenzi huyo alikuwepo akipitia vituo mbalimbali vya uandikishaji na kushiriki kutoa elimu ya mpiga kura na jinsi ya kuboresha taarifa kwa wananchi waliokuwa wamekuja vituoni kwa wingi.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera (aliyesimama) akitoa maelekezo kwa wananchi waliofika katika kituo cha Shule ya Sekondari Kisasa katika Kata ya Dodoma Makulu. Miongoni mwa wananchi waliofika kituoni hapo ni Dkt. Jabiri Bakari (mwenye shati jeupe) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA).
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera (kulia) akijibu maswali ya ufahamu kwa wananchi waliojitokeza kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kituo cha Shule ya Sekondari Kisasa kata ya Dodoma Makulu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.