Mhe. Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde akishiriana na wananchi wa Kata ya Makutupora kuchimba msingi wa madarasa katika Shule ya Msingi Veyula.
Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Ndejembi akikabidhi kwa niaba ya Mhe. Rais ahadi ya shilingi 10,000,000 kwa Mhe. Mbunge Mavunde.
Mhe. Mkuu wa Wilaya Deogratius Ndejembi na Mhe. Mbunge Anthony Mavunde akishirikiana na wananchi kuchimba msingi wa madarasa ya shule ya Msingi.
Wananchi wa Kata ya Makutupora walioitikia mwito wa kushiriki kuchimba msingi wa madarasa ili kusaidia ujenzi wa madarasa.
Mhe. Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akishiriki katika kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.
Mhe. Mbunge Mavunde katika kuitikia wito wa Mhe. Rais, amechangia shilingi 5,000,000 mifuko 100 ya saruji na kuahidi kiasi cha shilingi 5,000,000 zaidi.
Lt Col Matina Mkuu wa kikosi cha JKT Makutupora aliyekabidhiwa kusimamia kazi ya ujenzi ili ikamilike kwa wakati.
Mhe. Mbunge Mavunde na Mkurugenzi wa Jiji ndugu Godwin Kunambi wakijadiliana jambo ili kufanikisha kazi.
Mhe. Mbunge Mavunde akitoa nasaha zake baada ya zoezi kukamilika.
Mhe. Mbunge Mavunde amewasisitiza wananchi wa Jimbo lake kuwa mstari wa mbele katika kuchangia shughuli za maendelea ili kujiletea maendeleo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.