Serikali imetoa orodha ya watumishi wa umma waliokuwa na madai ya malimbikizo ya mishahara, baada ya kumaliza kufanya uhakiki wa madeni ya watumishi hao. Madeni hayo yatalipwa katika mshahara mwezi februari 2018.
Katika maelezo yake kwa vyombo vya habari leo mjini Dodoma kuhusu madai hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amesema Serikali kupitia mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara (Human Capital Management Information System – HCMIS) "Lawson" kufikia tarehe 01 Julai 2017 ilikuwa na madai ya malimbikizo ya mishahara yenye jumla ya shilingi 127,605,128,872.81 kwa watumishi 82,111. Madai haya yalikuwa ya muda mrefu mengine yakiwa ya kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2017
Aidha, Waziri Dkt. Mpango amesema kuwa hatua hiyo ni matokeo ya juhudi wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli kuwaondoa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara watumishi hewa, waliogushi vyeti na wasio na sifa ili kuboresha mazingira ya kazi na utendaji kazi katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.
Madai haya yalijumuisha mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za mishahara zilizotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishiwa mishahara.
Angalia hapa chini nyaraka zilizoambatishwa:
TAARIFA YA WAZIRI MPANGO KUHUSU MALIMBIKIZO MISHAHARA YA WATUMISHI.pdf
ORODHA YA MAJINA YA WATUMISHI WA UMMA WANAOSTAHILI KULIPWA MADAI YA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA.pdf
ORODHA YA WATUMISHI WA MANISPAA YA DODOMA WANAOSTAHILI KULIPWA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA.pdf
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.