Soko Kuu la Madini ya Dhahabu na Vito vya thamani Mkoani Dodoma linapatikana katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (mkabala na Benki ya NBC). Soko hili lilizinduliwa rasmi Mei 19, 2019 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge.
Aidha, Dkt. Mahenge alitoa rai kwa wachimbaji wadogo kuhakikisha wanatumia soko hilo kufanya biashara ya madini na kunufaika nalo. Pia aliwataka wafanyabiashara hao kuachana mara moja na kufanya biashara haramu ya madini na kutorosha madini hayo au kukwepa kodi na kuonya kuwa kwa kufanya hivyo watakumbana na hatua kali za kisheria.
Kwa wafanya biashara wa madini soko hili linakuwa mkombozi wao kuepukana na matapeli wa madini ambao wamekuwa wakiwalaghai watu mbali mbali na kuwaibia vito vyao kwa kuwabadilishia na vipande vya chupa. Wananchi wote wana wajibu wa kulitumia soko hili kuepukana na matapeli wa madini kwa kuwa soko hili lina watumishi wataalamu wa serikali na vifaa thabiti vya upimaji wa madini.
Soko hili linatoa mwanya kwa watanzania wote kuwa na hakika na uhalali wa madini yao. Matumizi ya soko hili yatalilongezea taifa pato kutokana na kodi inayotozwa.
Bofya hapa kusoma Hotuba ya Ufunguzi wa Soko la Madini - Mgeni Rasmi Dkt. Binilith Mahenge: Hotuba Ufunguzi wa Soko la Madini na Vito vya thamani
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.