• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Tanzania haina mgonjwa wa Corona - Waziri Ummy

Imewekwa tarehe: March 2nd, 2020

Mpaka sasa Tanzania haina Mgonjwa wala mtu anayehisiwa kuwa na ugonjwa  unaosababishwa na kirusi cha Coromna (Hona kali ya mafua), hata hivyo  kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo hasa kibiashara na kijamii kati ya Tanzania na nchi za bara la Asia ikiwemo nchi ya China nchi yetu inakuwa katika hatari pia ya ugonjwa huo.

Haya yamesemwa na Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akitoa tarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa ugonjwa huo.

“Ugonjwa huu unasababiswa na kirusi jamii ya Corona na ni kipya “Novel (New) Corona virus 2019” (2019-nCOV) ambacho ni tofauti na virusi vingine vya jamii hiyo ambavyo viliwahi kusababisha milipuko ya ugonjwa uliojulikana kama ‘SARS-CoV’ mwaka 2003 na MERS-CoV Corona Virus mwaka 2013”. Amesema Waziri Ummy.

Aidha, waziri Ummy amesema ugonjwa huo huambukizwa kwa njia ya hewa kwa kuingiwa na majimaji yenye virusi kutoka mtu mmoja kwa njia ya kukohoa au kupiga chafya au kwa kugusa majimaji au makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na dalili za ugonjwa huo na dalili huanza kuonekana kati ya siku moja hadi kumi na nne tangu kupata maambukizo.

Hata hivyo ametaja dalili za ugonjwa huu ni pamoja na Homa, mafua, kuumwa kichwa, mwili kuchoka, kikohozi, kubanwa mbavu, maumivu ya misuli, vidonda vya koo, mapafu kuathirika, kupumua kwa shida na hata kifo.

“Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja, hivyo kama yalivyo magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi, matibabu hufanyika kwa kuzingatia dalili zilizopo na ufuatiliaji wa karibu” Amesisitiza Waziri Ummy.

Wakati huo huo waziri huyo amewashauri wananchi kuchukua hatua ili kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuzingatia kanuni za afya na usafi ikiwa ni pamoja na kukaa mbali na mtu mwenye dalili za mafua mwenye historia ya kusafiri katika nchi zilizokumbwa na mlipuko na kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kitambaa safi au nguo uliyovaa sehemu za mikono

“Kutokana na mwenendo na kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huo kipindi hiki cha mlipuko, Wizara inashauri kusubiri na kuepuka safari zisizo za lazima kwenda kwenye maeneo yaliyoathirika na inapolazimu kusafiri basi wapate maelezo ya kitaalamu kabla ya kuondoka nchini pamoja na kuepuka kugusana na mgonjwa mwenye dalili za magonjwa ya njia ya hewa”.

Vile vile wananchi wanatakiwa kutoa taarifa ya uwepo wa mtu mwenye dalili zinazohisiwa kuwa za ugonjwa huu kwenye kituo cha huduma za afya kilicho karibu nawe au piga simu namba 0800110124 au 0800110125 bila malipo.

Kusoma taarifa kamili kwa umma bofya hapa: Tanzania haina mgonjwa wa CORONA

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliojitokeza tarehe 29/02/2020 kusikiliza tamko la Wizara kuhusiana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona uliotokea China na kutoa taarifa za Tanzania ilivyojiandaa katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo nchini. Kushoto ni Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile na kulia ni Mkurugenzi wa huduma za Dharura na Majanga Dkt. Elias Kwesi.

Chanzo:afyablog.moh.go.tz

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.