Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametoa taarifa ya wagonjwa waliothibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona katika Maabara Kuu ya Taifa leo tarehe 30 Machi, 2020.
"Ninapenda kutoa taarifa kwamba leo 30 Machi 2020 tumethibitisha kuwepo kwa wagonjwa wapya watano (5) wa COVID-19 baada ya kufanyikwa vipimo katika Maabara yetu Kuu ya Taifa. Kati ya wagonjwa hawa, watatu (3) ni kutoka Dar es Salaam na wawili (2) kutoka Zanzibar, ambao taarifa zao zitatolewa na Waziri wa Afya Zanzibar./
Hivyo sasa jumla ya wagonjwa wa COVID-19 nchini ni kumi na tisa (19) akiwemo mgonjwa mmoja aliyetolewa taarifa na Waziri wa Afya wa Za/nzibar tarehe 28/03/2020" amesema Waziri Ummy.
Mchanganuo wa taarifa ya wagonjwa wapya wa Dar es Salaam ni kama ifuatavyo:
Vilevile, Waziri Ummy amekazia kuwa "Kazi ya kufuatilia watu wote wa karibu waliokutana na wagonjwa hawa inaendelea (contact tracing). Aidha tunasisitiza na tunawataka wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari ili kujikinga na ugonjwa huu".
Kuisoma taarifa kamili bofya hapa: Taarifa ya Waziri Ummy ya wagonjwa wa corona 30 Machi 2020
Chanzo: wizara_afyatz (Instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.