Leo 27/03/2017, Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wamezindua tovuti mpya za Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, na Halmashauri zake zote 185 ikiwemo Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa nchi OR-TAMISEMI, Mh. George SImbachawene, na kuhudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe, Mkurugenzi Msaidizi wa USAID Tanzania, Tim Donnay, ambao ndio wafadhili wa Mradi wa PS3, baadhi ya Makatibu wakuu wa wizara, wakuu wa mikoa, maafisa TEHAMA na maafisa Habari.
Ujue Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) katika utoaji wa taarifa kwa umma.
Zabibu ni kati ya mazao ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ni alama ya manispaa ya Dodoma. Zao hili limeinua uchumi wa wananchi wengi vijijini wanafanya kilimo cha kisasa cha zabibu.
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.