Jiji la Dodoma limeendelea kutoa elimu ya chanjo ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19) na safari hii maafisa kutoka Jiji la Dodoma wamefika katika Kata ya Kikombo kutoa elimu hiyo kwa wananchi.
Waumini Anglilkana wahamasishwa kuhusu chanjo ya Korona.
CHANJO ya ugonjwa wa Uviko-19 ni muhimu kwa sababu inazuia kwa asilimia kubwa mtu asipate maambukizi na kuugua kufikia kiwango cha kuwekewa hewa ya ‘Oxygen’.
Kauli hiyo ilitolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method alipokuwa akitoa elimu na kuhamasisha watumishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) kwenye Bonanza la Wafanyazi Kujenga Afya lililofanyika katika uwanja wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dodoma.
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.