MWAKILISHI wa Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Mhe. Sospeter Mazengo amewakambidhi washindi wa mashindano ya UMISETA ngazi ya wilaya kwa upande wa mpira wa miguu na pete. Zawadi hizo zimetolewa katika uwanja wa mpira wa Shule ya Sekondari Dodoma.
Zawadi hizo amezitoa kama pongezi kwa timu ya mpira wa miguu na mpira ya pete lengo likiwa ni kuwapongeza na kuwafanya waongeze juhudi zaidi katika mashindano mengine yatakayokuwa yanaendelea.
Mazengo amesema michezo ni kitu kizuri kwakuwa inaburudisha na pia michezo ni ajila, watu wengi wameweza kuajiliwa, pia michezo ni afya inafanya wachezaji wawe na afya njema, hivyo ni vyema wanafunzi wakashiriki katika michezo kwa kuwa ina faida nyingi.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka amepokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Dkt. Binilith Mahenge aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Hafla ya makabidhiano ya Ofisi hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita tarehe 21 Mei, 2021 ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kuhudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Taasisi zilizopo Mkoani Dodoma, Viongozi wa Dini na wawakilishi wa Wazee wa Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 katika Mtaa wa Ndachi na kuwawezesha wananchi kupata hati za kumiliki maeneo yao kwa mujibu wa sheria.
Mkurugenzi Mafuru ametatua mgogoro huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa michezo katika Mtaa wa Ndachi uliopo Kata ya Mnadani jijini hapa. Mafuru amefafanua kuwa wananchi hao wamekosa maendeleo kwa muda mrefu kutokana na kuwa na migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu.
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.