MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema kuwa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma watarajia kumpa zawadi Mhe. Rais Samia kwa kumaliza jengo la kisasa litakalotumiwa na wafanyabiashara wenye biashara ndogo (almaarufu kama wamachinga) ifikapo tarehe 17 Machi, 2022 ambapo Mhe. Rais Samia atakuwa anatimiza mwaka mmoja tangu achukue nafasi ya kuongoza nchi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kazi nzuri inayoendelea katika ujenzi wa jengo la kisasa la wazi la wafanyabiashara wa biashara ndogo (Machinga) likiwahakikishia eneo salama la kufanyia biashara zao.
Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka alipoongoza Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Dodoma na viongozi wa Chama cha Mapinduzi ngazi ya mkoa kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo katika eneo la Bahi road leo.
Mtaka alisema “tunawapongeza sana Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kazi nzuri. Naibu Meya peleka salamu kwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma na madiwani kwa kazi nzuri. Mkurugenzi wa Jiji tunakupongeza sana. Mradi huu ni kielelezo kwamba una uwezo mkubwa wa kuongoza katika nafasi yako”.
Jiji Dodoma latatua changamoto ya eneo la 'Machinga'.
DC Shekimweri aanika na maazimio ya kusaidia
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.